Mbwa Wakali Zaidi Ambao Hufai Kuwapa Mafunzo Au Kuishi Nao Peke Yako

14674

Mbwa wanajulikana ulimwenguni kama rafiki mwaminifu zaidi wa binadamu. Ni ukweli, lakini kumbuka, jambo hili kwa ukubwa linategemea jinsi unavyoishi au kukaa na mbwa mwenyewe au wenyewe kulingana na idadi yao. Pia, ni muhimu kuelewa kuwa mbwa hawafanani wote. Kuna aina mbali mbali na wote wana tabia za kipekee. Kwa mfano, aina ya mbwa ajulikanaye kama Golden Retriever ni maarufu kwa ukubwa na uaminifu wake. Mbwa hawa wenye manyoya ya rangi ya dhahabu pia husaidia sana katika kazi za nyumbani. Pia, kuna wengine kama mbwa aina ya Rottweiler ambao wanaweza kupewa mafunzo lakini wanaweza kuwa wakali sana na pia hatari wasipopata mafunzo ya kutosha wakiwa wachanga. Kwa hivyo, iwapo una mipango ya kumleta mbwa nyumbani mwako unapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mbwa ili kuelewa ni mbwa yupi atakuwa bora zaidi nyumbani mwako.

1. Doberman

This image has an empty alt attribute; its file name is 1-1.jpg
germanshepherdtraininginfo.com

Mbwa huyu anayejulikana kama Doberman ni mwaminifu lakini pia anaweza kuwa mkali sana. Kwa sababu hizi mara nyingi yeye hutumiwa na polisi. Kando na kuwa mwerevu na mwaminifu, mbwa huyu wa aina ya Doberman huwa na ujasiri mwingi sana. Huwa hawapendi wageni. Mbwa huyu pia huwa mdadisi. Wana miili miembamba na kwa sababu hiyo wanaweza kufukuza watu kwa urahisi sana.

advertisement

1 / 30